CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimemshukia Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta, kikisema kiongozi huyo si mwadilifu, si mwaminifu na mnafiki, akiwa ni mwakilishi na kielelezo cha mfumo uliooza katika serikali ya CCM uliolifikisha taifa hapa lilipo.
Kimesema kuwa tabia za Sitta hasa katika kuua mijadala ya kifisadi ndani ya bunge, kwa ajili ya kulinda maslahi yake binafsi ya kusaka vyeo, inamfanya asiwe tofauti na watuhumiwa wengine wa ufisadi ndani ya chama chake na serikalini, kikishutumu kuwa mlinda ufisadi na mafisadi ama ni naye ni fisadi kama wenzake au ni fisadi mkubwa kuliko mafisadi wenyewe.
Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari mjini Iringa jana Ijumaa, Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dkt. Willibroad Slaa alisema kuwa Sitta hana uwezo wowote wa kukisema chama hicho wala viongozi wake, akimtaka amalize kwanza matatizo waliyonayo yeye na wenzake ndani ya CCM, likiwemo la kujivua gamba, ambalo linaonekana kuwashinda.
Katika mkutano huo chama hicho kilisema pia kuwa hatua ya polisi kuzuia mikutano ya Operesheni Sangara-M4C kwa siku tano, kupisha shughuli ya sensa, kumekisaidia chama hicho kugundua mbinu na mikakati mizuri ya kuwafikia wananchi kwa mikutano ya ndani, ikiwa ni maandalizi ya mikutano ya hadhara, hivyo kupata mafanikio zaidi mkoani Iringa kuliko ilivyokuwa mkoani Morogoro.
Sitta ni kielelezo
Katibu Mkuu huyo wa CHADEMA ambaye aliwaambia waandishi wa habari kuwa amelazimika kumzungumzia mtu lakini kwa nia ya kuonesha alivyo kielelezo cha ubovu wa mfumo na uongozi wa serikali na CCM, alidai kuwa kwa sababu ya tabia ya unafiki aliyonayo Sitta, kiongozi huyo ni sawa na viongozi wengi wa serikali ya CCM akiwafafanisha na mbwa mwitu waliovaa ngozi ya kondoo.
“Nchi hii imefika hapa ilipo kwa sababu ya viongozi aina ya Sitta ambao hawasiti kusema uongo hadharani, wanafiki, hawana uadilifu, waongo, walio tayari kusaliti maslahi ya umma kulinda maslahi ya tumbo, Sitta yeye ana uzoefu gani, huu wa kulinda mafisadi bungeni kwa kupindisha hoja za ufisadi ili apate ubunge na uspika.
“Hivi Sitta atuambie anaposema CHADEMA haina watu wenye uwezo lini tuliwahi kusema tukiingia serikalini tutakuja na watu wetu wote au ndiyo yale mawazo ya kijinga kwamba CHADEMA wakishika nchi watapata wapi ikulu…atuambie kuna chuo kikuu chochote kinafundisha uwaziri au kuna chuo kikuu kinafundisha ukatibu mkuu wa wizara, asitupangie sisi namna ya kupata viongozi wetu.
“Hivi hajui kuwa Mwalimu alipopata nchi aliandaa watendaji. Hoja za kipuuzi, mtu akitoa hoja za kipuuzi, naye atakuwa mpuuzi tu wa kupuuzwa, tumefika hapa, nchi imegubikwa na uozo wa ufisadi kwa sababu ya mawaziri wa aina ya Sitta ambaye haogopi kuropoka hadharani, tena akiwatukana wapiga kura, ambao pia wengi wao ni vijana.
Hoja ya kuchezesha disko
“Anaposema Mbowe ni mchezesha disko anataka kupeleka ujumbe gani, anataka kusema nini…kwamba ni kosa, kwa hiyo anamaanisha wacheza disko ni criminals (watenda jinai), kwa hiyo wacheza disko ambao pia ni wapiga kura na wengi ni vijana ni criminals, je hajui kuwa kuna mawaziri wenzake wanaokesha pale Billicanas Club,” alisema Dkt. Slaa.
Aliongeza kusema kuwa hoja hiyo ya kumshambulia Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe kwa sababu ya kumiliki ukumbi wa mziki, kuwa nayo ni hoja mbele ya watu makini, Dkt. Slaa alisema waziri huyo amedhihirisha alivyo mbumbumbu wa sheria na hajui lolote, tofauti na ambavyo siku zote ametaka kuonekana mbele ya jamii.
“Ni dhahiri hana uzoefu wowote na hajui, ndiyo maana ameishia kwenda kuwatukana wapiga kura yeye akifikiri anaimaliza CHADEMA, maana wacheza disko ndiyo wapiga kura hao hao, lakini yeye kama msomi kweli, tena anasema ni mwanasheria, alipaswa aelewe kuwa duniani kuna nyumba za disko za staha, zimesajiliwa na zinafanya kazi kwa mujibu wa sheria na zimepewa leseni na serikali.
“Huyu Sitta kila siku anajiita yeye mwanasheria kumbe mbumbumbu kupindukia tu hana tofauti na wana CCM wenzake ambao jamii inawashangaa kwa matendo na kauli zao, ku-run club ni sawa na ku-run biashara nyingine yoyote, almuradi iendeshwe kisheria na kihalali, sasa kama anaona ni kosa aiambie serikali yake ifute leseni ya biashara hizo.
“Tulitegemea mtu ambaye anataka kuonekana ni mstaarabu, anahoji uzoefu wa wenzake nay eye anasema ana uzoefu angekuja na mawazo ya kupeleka nchi mbele kumbe yuko sawasawa tu na wenzake ndani ya CCM,” alisema Dkt. Slaa.
Ameingia kichwakichwa, kwenye tope
“Leo nalazimika kumzungumzia mtu, Watanzania wanajua mara chache sana CHADEMA huwa tunalazimika kuzungumzia watu badala ya masuala…lakini nitazungumza kwa namna ambayo huyo mtu atakuwa anawakilisha mfumo huu wa serikali ya CCM na chama chao jinsi ulivyooza na kutufikisha Watanzania hapa tulipo.
“Samuel Sitta ameingia kichwa kichwa kwenye matope ambayo hawezi kutoka wala kujinasua, muda mrefu tumemhifadhi lakini leo tutampiga ngumi za uso lakini kwa namna ambayo atakuwa anawakilisha mfumo huu uliooza…
“Ghafla tu ameamua kuibuka na kuzingumzia CHADEMA, badala ya kujenga chama chake, bila kujua amedhihirisha kuwa CHADEMA sasa ni tishio kwao, maana huwezi kuzungumzia kitu ambacho hakikuathiri, amedhihirisha namna ambavyo yeye wenzake sasa wanatapatapa kweli kwa sababu ya CHADEMA.”
Makombora zaidi; mlinda ufisadi na mafisadi
Dkt. Slaa alisema kuwa wakati chama hicho kilipoanza kuasisi hoja ya ufisadi nchini kikiwa mstari wa mbele kupiga vita kila aina ya ufisadi, Sitta wakati huo akiwa Spika wa Bunge, ndiye alikuwa mtu wa kwanza kuweka vikwanzo na vizingiti akilinda maslahi yake nay ale ya chama chake, badala ya maslahi ya wananchi.
“Yeye ndiye aliyepindisha hoja ya Zitto katika kashfa ya Buzwagi ambapo waziri alikuwa amesaini mkataba uliokuwa kinyume kabisa na maslahi ya nchi, tena akasaini nje ya nchi hotelini. Zitto aliposimama bungeni, Sitta badala ya kuangalia hoja hiyo kwa maslahi ya nchi, yeye na wenzake akaipindua kuwa Zitto amesema uongo bungeni.
“Huyu bwana hastahili hata kuwa waziri, anajidai yeye mpiganaji na mpambanaji, wapi? Katika hoja ile nani alikuwa mpiganaji Zitto au Sitta, akapindisha makusudi hoja ya ufisadi mkubwa wa Buzwagi kulinda maslahi anayoyajua mwenyewe. Wakamfukuza Zitto bungeni kwa miezi minne, baadae kelele zilivyozidi huku nje, wakaamua kumrejesha bungeni kimya kimya baada ya mwezi mmoja tu hivi.
“Lakini pia ni Sitta huyu huyu alizima hoja ya ufisadi wa BoT, mambo yote yale ya EPA, Kagoda, Deep Green sijui nini kila kitu kilichokuwa kikihusu BoT. Mtakumbuka aliwatangazia Watanzania kuwa nyaraka za Dokta Slaa ni fake za kuokoteza kwenye internet na nitampeleka polisi, mpaka leo hakunipeleka. Lakini Sitta alikuwa anajua tangu mwanzo, kadri nilivyokuwa nikikusanya documents alikuwa anajua na nampatia copy, mpaka ikafikia ile document kubwa ya mwisho.
“Lakini kwa unafiki wake ameahirisha bunge Ijumaa, Jumamosi akachukua ile document na kwenda nazo TBC akisema ni fake na atanipeleka polisi, lakini leo yako wapi…sasa mtu wa namna hii hafai hata kuwa naibu waziri, mtu yeyote anayelinda mafisadi na ufisadi ni fisadi kuliko mafisadi wenyewe, nawaambia haya kwa sababu tumefika hapa kwa sababu ya kuwa na viongozi, wakiwemo mawaziri wanafiki na waongo kama hawa.
“Lakini ili mjue Sitta ni mtu wa aina gani na kwamba hastahili kuaminika na Watanzania, haikuishia hapo, ufisadi wa Richmond mnajua alivyomaliza mjadala ule kihuni bungeni. Hadi leo hoja ile haina majibu, wakati tunahoji bungeni akafunga hoja ile kidikteta, sasa tunauliza huo ndiyo uzoefu alionao yeye au walionao wenzake, uzoefu wa kulinda mafisadi na ufisadi wa CCM na serikali yao, lakini sisi tunajua kwa nini alipindisha hoja ya Richmond, wakati huo alikuwa anabembeleza ili ateuliwe kuwania ubunge na baadae uspika, mnaona huyu ni mtu wa kuaminika kweli?”
“Hivi kwa matendo ya aina hii Sitta anaweza kutoka nje na kusema yeye ni jasiri na mzalendo, katika majasiri na wazalendo wa kweli Sitta hana sifa hizo, ndiyo maana wameshindwa hata kuyavua magamba kama walivyosema, sasa aende kwanza kwenye chama chake na serikalini, asaidie kuyaondoa magamba kabla hajaanza kutafuta aibu ya kuanikwa zaidi,” alisema Dkt. Slaa.
Siri zaidi; Sitta haaminiki
Dkt. Slaa aliongeza kusema kwa kutoboa siri zaidi namna ambavyo, yeye na Mwenyekiti wa CHADEMA Mbowe, walikuwa wakiendesha mazungumzo na Sitta wakati mwingine kwenye Ofisi ya Spika juu ya Sitta kuhamia CHADEMA na kuwania urais katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2010, akisema kuwa ulikuwa ni wakati ambapo waziri huyo pamoja na wenzake walipokuwa wameunda Chama Cha Jamii (CCJ) wakiwa bado wako CCM.
Alisema kuwa hata wakati huo bado Sitta alikuwa akionekana kutojiamini na maamuzi yake, ambapo wakati wa majadiliano ya kugombea urais, Sitta alisema kuwa kuna kundi la wabunge takriban 55 watiifu kwake ambao walikuwa tayari kuhama naye kumfuata CHADEMA.
“Leo natoa siri ambayo sijawahi kuitoa, Sitta ni mhanini. Tumekutana naye mara 100 na zaidi, tumeandikiana vimemo bungeni vya kukutana, wakati mwingine tumekutana hata Speaker’s lounge, tumekutana na Sitta na Mwenyekiti Mbowe, ambaye leo anamwita ni mchezesha disko mara nyingi tu. Lakini hata wakati huo pia hakuonekana kuwa jasiri, maana alikuwa ana wasiwasi nani wanamfuatilia au nani wanamuona, si mtu jasiri hivyo.
“Zikiwa zimebaki kama siku tano kabla ya kumaliza bunge la mwezi wa saba, kila nikimwandikia kimemo, hataki hata kunitazama, Sitta akayeyuka bila hata kutuaga, baadae CHADEMA tukaamua kutumia utaratibu mwingine na tukaweza kusonga mbele mpaka kufika pale tulipofika. Lakini baada ya uchaguzi akaja mwenyewe kunifuata akinishukuru sana na kunipongeza kuwa nilikuja na hoja tofauti kwenye uchaguzi akisema hata yeye asingeweza kufika tulipofika.
“Lakini hapo sasa tulishamshtukia na kugundua kuwa anataka kugombea uspika kupitia CHADEMA, nataka kuonesha namna huyu mtu alivyo mnafiki, mpotoshaji, nampatia challenge kama kweli yeye ni muumini mzuri akanushe haya, maana ametulazimisha kusema, kwa hoja zake za kupotosha watu na akumbuke, maana huwa anakwenda makanisani na anachanga mapesa, akumbuke maandiko yanasema, yeyote atakayepotosha wadogo hawa, anastahili kutoswa baharini, Makamu Mwenyekiti hapa ametumia Quran kufafanua vizuri,” alisema Dkt. Slaa.
“Maana kwa hakika anataka kupotosha watu ili waone kuwa kuchezesha disko ni suala lisilokuwa sahihi, huo ni upotoshaji, kama anataka kuonesha si sahihi mbona serikali yake hiyo hiyo inaendelea kukusanya kodi. Sasa ilipofikia kwenye suala la kugombea uspika, siku ile jina lake limekatwa kwa sababu walitaka mgombea mwanamke, alinipigia simu usiku wa saa tisa, bahati mbaya nilikuwa nimeweka simu silence, hakunipata.
“Saa 12 nikapokea simu ya mke wake, Margreth Sitta, anasema baba anakutafuta tangu usiku, anataka kuzungumza nawe, nikasema sawa, akaniambia Dokta Slaa wamenifanyia kitu kibaya sana, mimi nimeamua sasa nitagombea uspika kwa tiketi ya CHADEMA, najua umeshateua tayari mtu wa kugombea tayari, lakini naomba nikuhakikishie nafanya press conference saa 4 asubuhi leo, natangaza rasmi kugombea uspika kupitia CHADEMA. Nikamjibu CHADEMA maamuzi hayafanywi na mtu mmoja, nikamwambia asubiri niwasiliane na Mwenyekiti wangu wa chama.
“Baadae tukakubaliana tukutane nyumbani kwake, lakini akawa anasema tusubiri kwanza anamalizia kupanga mikakati na wabunge 55 wa CCM, lakini akisisitiza kuwa uamuzi wake uko pale pale, nikamuuliza vipi kuhusu press conference mbona muda unakaribia, akasema hakuna shida yeye atatuma tu watu wake wataitisha haraka, akasema lakini wanataka kumpatia unaibu waziri, hivyo bado anasumbuana nao, kengele ikalia kichwani sasa huyu mtu akipewa uwaziri itakuwaje.
“Baadae ananiambia, Dokta Slaa nimepigiwa simu na bwana mkubwa naenda kuonana naye, tangu wakati huo Sitta akapotea mpaka saa 8 ndiyo anapatikana, akaanza kuniambia ni lazima aende kwanza Urambo kuwaaga wazee, maana hawezi kuhama bila baraka zao, nikamuuliza vipi kuhusu press conference akasema tutaifanya Jumatatu ijayo Dar es Salaam, akaniambia; tena saa 9 uje uone statement ambayo nimeshaiandika ili na wewe uongeze inputs, Sitta huyu akaniambia kuwa Anne Makinda hatakaa zaidi ya miezi sita kwenye kiti cha uspika.”
Dkt. Slaa alisisitiza akisema kuwa nchi imefika hapa ilipo ikiwa imegubikwa na uozo wa ufisadi kila kona, ukiongeza idadi ya maadui wa taifa, kutoka watatu hadi wanne (umaskini, ujinga, maradhi na ufisadi/CCM) kuanzia ngazi ya chini hadi juu, kwa sababu ya ukosefu wa uadilifu, uaminifu kama Waziri Sitta.
Atalipuliwa zaidi
Dkt. Slaa alisema kuwa ameamua kuzungumza hayo machache kwa sasa, lakini ataongeza ‘kumlipua’ zaidi Sitta endapo atajitokeza kujibu haya ya sasa.
“Yeye ana uzoefu gani Sitta, hana uadilifu, si mwaminifu, nchi hii imeoza kwa sababu ya viongozi ya aina ya Sitta, nataka ajibu kwanza hayo kisha nitamlipua zaidi. Ana uadilifu gani katika nchi hii, ametumia mabilioni ya hela ya walipa kodi wa Tanzania kujijengea Ofisi ya Spika Urambo, tunauliza kuna spika wa Urambo au alijua yeye atakuwa spika wa milele au basi Makinda awe anakwenda Urambo wakati wa mapumziko ya bunge.
“Tulichoamua bungeni ni kwamba kila mbunge ajengewe ofisi yenye thamani isiyozidi milioni 40, lakini yeye akaenda kujijengea ofisi ya milioni 350 tena kwa kasma tofauti na inavyotakiwa lakini kibaya zaidi tendering process ya vifaa vya ofisi haikufutwa na vililetwa na kampuni ambayo majuzi imehusishwa na Blandina Nyoni, hakuna mahali tendering imefanyika, amefanyia ufisadi mali ya taifa,” alisema Dkt. Slaa.
More still to come about the press conference...
![]() |
| Samuel Sitta mwenyewe anayepigwa mkwara na Guninita yupo hoi kwa usingizi.Labda hapo anaota yeye bado Spika |
Guninita ‘amvaa’ SittaPosted By admin On July 22, 2011 @ 7:59 am In Habari kuu,Mtanzania |• Adai ni mzigo, anawadanganya na kuwapotosha wananchi• Asisitiza ni sehemu ya tatizo la mgawo wa umeme• Asema si mgeni serikalini, ni mchochezi, mnafiki na mfitini• Aonya anaigawa, anaitumbukiza CCM kwenye shimo• Asema mambo yakiendelea hicho mwaka 2015 CCM itaambulia patupuNa Habakuki UrioMWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Dar es Salaam, John Guninita amemlaumu Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samwel Sitta akidai ni mnafiki na mchochezi anayetumika kuigawa CCM na kukitumbukiza chama hicho kwenye shimo.“Sitta ni sehemu ya serikali na si mgeni serikalini. Alikuwapo tangu kipindi cha Mwalimu Nyerere, na pia alikuwa Spika wa Bunge. Kwa nafasi hizi yeye ni sehemu ya tatizo na siyo kuwadanganya wananchi na kuwapotosha kwa kuirushia serikali lawama.‘Anaudanganya umma. Anataka kujenga umaarufu ambao siyo wa kwake. Kama ni kuharibu waliharibu wote na siyo kusema tatizo ni la serikali.‘Sitta amekuwa mchawi wa CCM… chama kinajimaliza chenyewe tena kwa kutumia viongozi wa nafasi za juu.,” alisema Guninita.Guninita alikuwa akizungumza katika mkutano wa hadhara Mbezi na Mbezi kwa Msigani katika jana, katika ziara ya kutekeleza agizo la Mwenyekiti wa CCM, Rais Kikwete la kuleta mageuzi ndani ya chama hicho na ‘kujivua gamba’.Alisema hali ya siasa ndani ya chama hicho si shwari kutokana na mgawanyiko mkubwa wa baadhi ya viongozi ambao wanazungumza wanavyojisikia bila kujali maslahi na ukweli ndani ya Chama hicho.“Kilichotufikisha hapa tulipo leo ni unafiki na fitina za viongozi kama Sitta ambao hawaeleweki wanafanya nini ndani ya chama chetu. Ndiyo maana viongozi wanajiuzulu ovyo, kitu ambacho siyo sahihi, chama kinapoteza makada muhimu na kuwaacha watu mizigo na wafitini.“Namshangaa Waziri Sitta, ana uwezo wa kwenda kwa Rais muda anaojisikia na pia alikuwa na nafasi ya kuyasema mambo yale katika vikao vya chana “party caucus”, na pia kwenye vikao vya Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) lakini anaropoka mambo kama hayo mbele ya umma wa watanzania na kuwapa umaarufu wapinzani.“Amekosa busara kwa kuwa amekiuka maagizo ya Rais. Tunajua hakutumwa na Rais, bali alikurupuka tu, na bila kujijua anaiponda Ilani ya Uchaguzi ya CCM ambayo ndiyo muongozo wa kutekeleza majukumu yetu.‘Mawaziri na wabunge wanasema tofauti na Rais anavyosema kuhusu matatizo ya umeme kwa sasa,” alisema GuninitaAlisema kauli mbovu za baadhi ya viongozi ambazo hazina ukweli zinabomoa chama, na kama CCM haitakauwa makini na kuwaonya wapotoshaji hao katika uchaguzi mkuu wa 2015 chama hicho kitaambulia patupu.“Upinzani wanajipanga vizuri katika kuhakikisha mwaka 2015 wanachukua nchi, na kwa hali hii tulio nayo … kwa kauli za akina Sitta watafanikiwa kwa kuwa chama kitakuwa kimeyumba na kukosa imani kwa wapigakura wake.“Haya siyo maneno ya Waziri, huyu jamaa ana mambo yake anayotekeleza… haiwezekani Sitta leo kuyasema haya, labda ana hasira za kukosa Uspika wakati yalikuwa makubaliano ya CCM kumuondoa kwa mafanikio ya chama na kutimiza sera ya 50 kwa 50.‘Nilimsikia akisema kuwa atatembea mikoa yote kulisema hilo, lakini nawahakikishia kuwa hatafika Dar es Salaam labda aje na barua ya Mwenyekiti au Katibu Mkuu wa CCM kuwa wamemruhusu kupotosha jamii. Nasema kuwa hatutakubaliana na uongo wake,” alisisitiza Guninita.Hivi karibuni, katika mkutano wa hadharani mjini Mbeya, Sitta pamoja na mambo mengine, alikaririwa akishauri serikali iwaombe radhi wananchi kutokana na tatizo la mgawo wa umeme unaoendelea nchini hivi sasa.Guninita alisema mkutano wa jana ni matunda ya makubaliano ya kujivua gamba kama alivyoagiza Mwenyekiti Kikwete na kuwataka viongozi wote wa CCM kutembelea matawi na mashina katika maeneo yao kuyajua matatizo ya wapiga kura wao na kuimarisha mizizi ya chama ambayo ipo katika mashina na matawi.
Salim Said
SPIKA wa Bunge Samuel Sitta amewashukia wana-mtandao wa asasi za kiraia zinazotetea usawa wa jinsia, haki za binadamu na maendeleo ya ukombozi wa Wanawake, akisema wanatia mashaka na kwamba wanaendeshwa na utashi binafsi wa wajanja wachache, huku wenyewe wakisema maandamano yapo palepale.
Wanaharakati hao, walitangaza maandamano makubwa ya amani yatakayoendeshwa nchi nzima kupinga kuvungwavungwa kwa hoja za mikataba ya Richmond, TICTS, TRL, taarifa ya uchafuzi wa mazingira kwa kemikali za sumu katika mgodi wa North Mara na ukiukwaji wa haki za binadamu, Loliondo.
Akizungumza na Mwananchi jana Spika Samuel Sitta alipingana vikali na madai ya wanaharakati hao, kuhusu Bunge na kueleza kwamba mtu yeyote akitaka kupima uwezo na uzuri wa bunge katika maamuzi na kusimamia serikali aangalie rekodi ya kazi za bunge kuanzi mwaka 2005 hadi sasa.
'Mimi sikubaliani na wanaharakati hawa hata kidogo. Maandamano ni haki yao na waandamane, lakini hawawezi kupima kazi za bunge kwa kuangalia kipindi cha mitafaruku ," alisema Spika Sitta.
Spika Sitta alisema kuimarisha Bunge si kazi ya lele mama, bali ni mapambano yanayohitaji ujasiri wa hali ya juu.
"Mimi naamini kwamba bunge letu limeimarika katika kuisimamia serikali ukilinganisha na lilikotoka, wanaharakati wanapaswa kujua pia kuimarisha bunge ni mapambano," alisema Spika.
Kuhusu suala la bunge la mfumo shirikishi wa demokrasia, Spika Sitta alisema hilo ni kinyume na katiba, lakini aliwataka wanaharakati hao wajaribu kujenga hoja.
"Mimi naona mfumo wa demokrasia ya uwakilishi bungeni ni mzuri tu, kwa sababu unapatikana kupitia uchaguzi ambayo ni ridhaa ya wananchi, lakini mfumo shirikishi utapatikana wapi.
"Huwezi kushirikisha mashirika au taasisi hizo katika bunge, kwanza zinamwakilisha nani, kwanza haziwawakilishi wanawake ni utashi tu wa baadhi ya wajanja," alihoji Spika Sitta.
Alisema mitandao hiyo inatia mashaka kwa wahisani kwani baadhi ya taasisi zinakula fedha bila ya kupeleka mrejesho kwa wahusika.
"Mambo yote ya bunge yanajadiliwa hadharani na kila mtanzania anayetaka anasikia, lakini je mambo ya hawa wanaharakati na mitandao yao yanajadiliwa na nani," alihoji Spika Sitta.
Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao wa Concern for Development Initiatives in Africa (ForDIA), Bubelwa Kaiza alisema ujumbe wao mkubwa katika maandamano hayo, ni kwamba hoja hizo zimevungwavungwa na bunge halitambui nguvu na mamlaka liliyopewa kikatiba, badala yake linafanya kazi kwa maslahi ya vyama vya siaasa na sio wananchi.
"Wapo wanaotaka tusiandamane, lakini huo ni woga wao tu, maandamano yapo palepale nchi nzima, tuna sababu za msingi za kuandamana kwani bunge halikuwajibika katika kushughulikia hoja mbalimbali katika kikao cha 18, badala yake limezivungavunga hoja hizo kwa maslahi ya vyama vyao vya siasa.
"Sisi pamoja na wananchi hatukuridhika kuhusu hoja zile zilivyohitimishwa, hakuna pia aliyewajibishwa, kwa hiyo tunaitaka serikali iachane na mfumo wa demokrasia wakilishi na ianzishe mfumo wa demokrasia shirikishi wa bunge ili wabunge waweze kuwajibika moja kwa moja kwa wananchi," alisema Kaiza.
CHANZO: Mwananchi

CHANZO: Mwananchi
Nadhani sasa kuna umuhimu wa kuangalia kama Spika huyu wa Viwango na Spidi bado anastahili kuendelea na wadhifa wake ambao ni wa nne kitaifa.Natoa hoja hiyo kwa vile kuna kila dalili kuwa Spika Samwel Sitta sasa anaogopa kivuli chake mwenyewe.
Ni hatari kwa kiongozi wa kitaifa kama Spika kutoa madai mazito namna hiyo pasipo kuwa na uthibitisho wowote.Hivi hao mafisadi wanaohatarisha maisha yake ni akina nani?Nauliza hivyo kwa vile kwa mujibu wa maelezo yake inaonyesha anawafahamu hata kwa majina.Sasa tunapokuwa na kiongozi wa kitaifa ambaye pindi maisha yake yanapokuwa hatarini (kama unaamini anachosema) anakimbilia kuomba aongezewe ulinzi hadharani,then hapo kuna mushkeli.
Ni hatari zaidi kumsikia Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,taasisi tukufu yenye jukumu la kutunga sheria za nchi,akiuliza bila aibui wala uoga "Hivi kama kweli nataka kuficha faili la Bunge nani anaweza kunizuia humu ndani?” You can't be serious,Mzee wa Spidi na Viwango!Yaani unatuambia kuwa kwa wadhifa wako unaweza kuficha nyaraka muhimu za Taifa (mfano faili la Bunge) na hakuna mwenye uwezo wa kukuzuia?Nadhani unatafsiri vibaya madaraka yako.Uspika ni nafasi inayoongozwa kwa taratibu na sheria,za nchi na za Bunge unaloongoza.Sasa unapotuambia kuwa hakuna wa kukuzuia ndani ya Bunge kuficha faili (ukijiskia kufanya hivyo) unatuaminisha kuwa aidha huelewi mipaka ya kazi yako,au unadhani Uspika ni kuwa juu ya sheria za nchi na Bunge,au kulewa madaraka.
Tukiwa hapohapo kwenye hoja yako ya "hakuna wa kukuzuia...",na tukiamini kuwa ni kweli hakuna wa kukuzuia,je utalalamika kuwa mafisadi wanakuwinda wakikuzushia zengwe kwamba umeficha nyaraka muhimu zaidi ya faili la Bunge?Sawa utasema wanakuandama lakini ushawapa hoja kwamba "ukitaka kuficha faili la bunge hakuna wa kukuzuia".Well,wao wanaweza kuja na tuhuma kubwa zaidi ya kuficha faili.Laiti busara zingetumika,ungeishia tu kukanusha tuhuma za kwamba una mpango wa kuchoma moto ofisi za bunge,na sio kukurupuka kudai una uwezo wa kuficha faili la bunge pasipo kuwapo wa kukuzuwia.
Ni rahisi kwa Spika kuomba aongezewe ulinzi (kwa kigezo kuwa ulinzi alionao sasa hautoshi) kwa vile gharama za kuongezewa ulinzi zitabebwa na walipa kodi na si kutoka mfukoni mwa Spika.Hoja hii ya Spika Sitta pia inaweza kufanya tujiulize iwapo licha ya nafasi yake ya Uspika,Mheshimiwa Sitta pia ni mtaalam wa mambo ya ulinzi wa viongozi,na review aliyofanya katika protection anayopewa hivi sasa imempelekea kuhitimisha kuwa ulinzi alionao hautoshi.Hii ni sawa na kuwadharau professionals wenye jukumu hilo,ambao naamini wangetambua mapungufu hayo kabla hata ya Spika Sitta kutamka hadharani.
Lakini twende mbali zaidi kwenye hili la "ulinzi alionao Spika hautoshi"Je anaweza kututhibitishia japo tukio moja linaloashiria kutotosha kwa ulinzi alionao hivi sasa?Yaani kutuhumiwa kuwa anataka kuchoma moto ofisi za bunge, na "maadui zake kumwaga fedha jimboni kwake" vimekuwa matishio ya kiusalama yanayotosheleza kufikia uamuzi wa kumuongezea ulinzi?
Kichekesho ni kwamba wakati Spika akimtaka Mbunge wa Cuf (Mheshimiwa Shoka Hamis Juma) afute kauli yake kwa kuwa "ushahidi aliotoa-katika madai kuwa kuna chama flani kinanunua shahada wakati wa chaguzi-ni dhaifu",yeye mwenyewe anafanya kilekile cha kutoa madai dhaifu kuwa nguvu ya mafisadi inahatarisha usalama wake ilhali hajaweza kutoa uthibitisho wowote zaidi ya "kauli za kisiasa" kuwa maadui zake wanapeleka pesa jimboni kwake ili asirejee bungeni.Ana uhakika gani kuwa hao anaowaita maadui zake si wananchi wenye dhamira ya kuleta maendeleo katika jimbo hilo pasipo kuwa na ajenda za kisiasa?Au Spika Sitta anataka kutuambia kuwa ni yeye tu aliye na hatimiliki ya kupeleka misaada katika jimbo hilo?Jamani,yaani hadi maendeleo ya jimbo yanafanywa kuwa mithili ya maamuzi ya mtu binafsi!?
Kuna mengi ya kujadili kuhusu kauli za Spika Sitta,lakini lililo wazi ni kwamba nafasi anayojipachika ya ukinara wa mapambano dhidi ya ufisadi ni sawa na political conmanship.Kwa lipi hasa?Sio Sitta huyu aliyempa "kifungo" Zitto Kabwe kwa "kosa" la kumkalia kooni Karamagi kuhusu Buzwagi?Sio Spika Sitta huyu aliyetishia kumfungulia mashtaka Dkt Wilbroad Slaa pale mbunge huyo wa Karatu aliposhikilia bango kuhusu ishu za ufisadi?Ni lipi alilofanya Samweli Sitta,kama Spika wa Bunge la Jamhuri au Mbunge wa Urambo linaloweza kumjumuisha kwenye kundi la vinara wa mapambano dhidi ya ufisadi?Yaani Watanzania wenzake kutamani jimbo la Urambo imekuwa ufisadi?Au mtu kutamani nafasi ya uspika imekuwa ufisadi?
Lakini kwa vile siasa zetu kwa sasa zinaruhusu mambo ya ajabu kabisa kutokea,kauli hizi za Spika Sitta hazitawahangaisha wenye dhaman ya uchambuzi wa kauli hatari kama hizi na kuchukua hatua za haraka.Ni business as usual,kauli imetolewa,siku imepita,and life goes on!
Na kwa vile magazeti yetu yako bize zaidi kuripoti habari badala ya kuchambua mantiki ya habari husika,yayumkinika tutasikia makubwa zaidi ya kauli hizi za wanasiasa wanaoogopa vivuli vyao wenyewe.Na kwa vile kilio,kicheko,kuchafua hewa na hata kukoroma kwa mwanasiasa kunatosha kuwa leading news kwenye magazeti yetu,basi tutarajia vimbwanga zaidi.
Trust me,tutashuhudia vituko vingi zaidi na zaidi kadri siku zinavyoyoyoma kuelekea uchaguzi mkuu wa 2010.By the way,si ndio tunaelekea kile kipindi cha usanii wa kisiasa ambapo watu wazima hupiga magoti majukwani na wengine kutoa shikamoo hata kwa watoto wadogo alimradi wahakikishiwe kura?
KINACHOKWAMISHA VITA DHIDI YA UFISADI NI HUU MTINDO WA KUENDESHA MAMBO KISHKAJI.UKITAFAKARI KAULI YA CHEYO KUHOFIA KUHUSISHA HABARI ZA UFISADI HUO NA HATUA YA SPIKA KUMTOA NJE YA BUNGE HIVI KARIBUNI UTAGUNDUA KUWA BADALA YA MBUNGE HUYO KUSHUGHULIKIA SUALA HILO KAMA MWENYEKITI WA KAMATI HUSIKA,YEYE ANAJIONA KAMA JOHN MOMOSE CHEYO ALIYETOLEWA NJE NA SAMUEL SITTA,BADALA YA OFISI YA BUNGE ILIYO CHINI YA SPIKA NA WATENDAJI KADHAA.
NA UNAFIKI MWINGINE NI WA HAO WABUNGE WALIONUKULIWA KATIKA HABARI HII AMBAYO HAWATAKI KUTAJWA MAJINA KISA WANAOGOPA KUANDAMWA NA WABUNGE WENZAO.KWANI WALIINGIZWA BUNGENI NA HAO WABUNGE WENZAO WANAOWAOGOPA AU WANANCHI HUKO MAJIMBONI?
WIZI MTUPU!
Subscribe to our newsletter to get the latest updates to your inbox. ;-)
Your email address is safe with us!