Featured Posts

Saturday, November 28, 2009

JK AOMBA UJUZI WA REGGAE JAMAIKA


KINGSTON, Jamaica

RAIS Jakaya Kikwete ametaka ushirikiano zaidi kati ya Jamaica na Tanzania katika nyanja za muziki na michezo.

"Jamaica ina wanariadha wenye kasi zaidi duniani kwa sasa," alisema kwa kusifia.

Alisema kuwa muziki wa rege ni maarufu zaidi nchini Tanzania, huku akimtaja nyota wa muziki huo, Bob Marley kuwa ni maarufu zaidi nchini mwake.

Kikwete aliiomba Jamaica kuisaidia nchi yake kwa kuwapatia kocha wa ajili ya kuendeleza mchezo wa riadha.

Kiongozi wa Upinzani, Portia Simpson Miller alimweleza Kikwete kuwa wanachama wa chama chake, People's National Party nao wako tayar kushirikiana na Tanzania.

CHANZO: Mwananchi

Alimshauri rais aanzishe ofisi nchini kuratibu shughuli za ushirikiano katika ukanda wa Karibiani.

0 comments:

Post a Comment

 
Design by Free WordPress Themes | Bloggerized by Lasantha - Premium Blogger Themes | Hot Sonakshi Sinha, Car Price in India