Featured Posts

Saturday, September 18, 2010

Hii Sasa Balaa: Sala Ya Baba Yetu Kikwete


Sijaitunga mimi,nimeipokea tu,nikasioma na kuisambaza

Ee KIKWETE Uliye tufilisi, 
Jina lako USANII MTUPU, 
utakalo lifanyike BAGAMOYO TU,
utupe leo mabilioni yetu ya EPA, uwapeleke MAFISADI wote Mahakamani, 
uwape WASTAAFU pesa zao, 
uwasamehe wafungwa hasa BABU SEYA kama ulivyomsamehe LOWASA, 
Usitutie katika mikataba FEKI,
 kwa kuwa UFISADI ni fani yako na uwongo hata milele, 
na Uanguke kwenye uchaguzi ujao kama unavyoanguka hovyo jukwaani, AMINA 


UPDATE: Nimetumiwa Sala nyingine,hii inamhusu Dokta Slaa,nimeisoma na kuisambaza



""IMANI YA CHADEMA""
Namwamin Dk.WILBROAD, mwana wa SLAA, Ndugu Yetu, aliyepitia vikwazo vingi kwa hujuma za CCM. Akateswa kwa kashfa za Ndoa, Akadhihakiwa, Akapingwa, Akaonyesha msimamo; Siku ya siku akasimama kwa kishindo; Akapaza sauti, Ameketi mkono wa kuume kutetea haki za Watanzania; Kutoka huko atakuja kuwahukumu mafisadi.

6 comments:

La Princessa said...

hahhahhahah!!!!

Anonymous said...

mungu ampe afya kikwete atuongoze milele

Anonymous said...

Afya yakutuongoza milele ampe mungu au walinzi wake anaopewa na Sheikh Yahya Hussein? Mbona mnachanganya mambo?? By the way kuongoza milele hawezi maana ata Mobutu Seseseko hakuweza kuongoza milele. But the prayer is interesting!

Chacha o'Wambura a.k.a Ng'wanambiti! said...

Sala zote zina mantiki!

SIMON KITURURU said...

:-)

OUR DIARY said...

Ha ha I love politics with all my soul,mind and heart.. The prayers are too funny Btw,
THIS YEAR IS FOR DR. SLAA..GOD BLESS TZee..

Post a Comment

 
Design by Free WordPress Themes | Bloggerized by Lasantha - Premium Blogger Themes | Hot Sonakshi Sinha, Car Price in India