Featured Posts

Sunday, March 20, 2011

Picha Hii ni Maalum kwa Mafisadi


Pichani ni hekalu linalomilikiwa na Dikteta Muamar Gaddafi.Jumba hilo la kifahari (thamani yake ni takriban shilingi bilioni 27)lipo jijini London lakini kwa sasa limepata "wamiliki" wapya...watu wasio na makazi maalumu (squatters) wameamua kuchukua sheria mkononi na kuhamia hapo.Nani asiyetaka kuishi kwenye hekalu?Na hasa pale mmiliki wa hekalu hilo maji hana hakika kama kesho atakuwa madarakani!!!

Je mafisadi wanapoona picha kama hii viroho haviwadundi japo kidogo?Good news is,hata wasipokumbwa na kimbembe kama hiki cha Gaddafi,siku moja wataitwa mbele ya haki na Mwenyezi Mungu...na hayo mabilioni wanayotudhulumu,kutunyang'anya,kutuibia,kutupora,nk WATAYAACHA HAPA HAPA DUNIANI.

2 comments:

LIFEOFMSHABA said...

VIONGOZI WA AFRICA WOTE WEZI TU

Anonymous said...

Tunayasubiri majengo ya ROstamu na maswaiba wake tutayageuza shule za chekechea za swahili medium

Post a Comment

 
Design by Free WordPress Themes | Bloggerized by Lasantha - Premium Blogger Themes | Hot Sonakshi Sinha, Car Price in India