Makala yangu ndani ya toleo la wiki hii la gazeti la Raia Mwema inazungumzia UNAFIKI: Ule wa Profesa Mwandosya kuitaka Dawasco isiwataje hadharani mawaziri wanaodaiwa maji na Mamlaka hiyo;ule wa Askofu Thomas Laizer wa KKKT Dayosisi ya Arusha kutumia neno la Bwana kuwapiga vijembe wanamwandama Lowassa,na ule wa "mabilioni ya EPA yanayorejeshwa kwa kasi."Makala hiyo imeanza kwa stori za hapa na pale,mambo ya muziki wa kufokafoka na albamu ya Jay-Z ya American Gangster ilivyosahau matatizo ya Black Americans.Stori hizo ni zinaunganishwa katika namna ile ile ya conversational style,napenda sana makala iwe mithili ya kupiga stori na msomaji,iwe kijiweni,kwenye pub,au hata barazani.Pamoja na habari na makala zilizokwenda shule,bingirika na makala hiyo kwa KUBONYEZA HAPA

KATIKA PICHA YA CHINI,KUSHOTO NI DADA TUNU,MKE WA WAZIRI MKUU MPYA MIZENGO PINDA.NI NDOTO AMBAYO KILA MKE ANGEPENDA IWE KWELI KATIKA MAISHA YAKE YA NDOA.HAPA NDIPO UAMUZI WA KUSEMA I DO UNAPOONEKANA WA BUSARA KULIKO MAAMUZI YOTE MAISHANI

Mwezi Novemba mwaka 2006,niliandika makala moja iliyotoka katika gazeti la KULIKONI (toleo la tarehe Novemba 3-9, 2006 2006).Katika makala hiyo (BONYEZA HAPA KUISOMA),nilizungumzia kusikitishwa kwangu na habari kwamba ex-PM Edward Lowassa alikuwa akifanya jitihada za kuwanyamazisha wabunge wa CCM kuhusu shinikizo la kujadili mkataba wa Richmond.Pia katika makala hiyo nililaumu staili ya uongozi wa Lowassa ya kuwaumbua hadharani watendaji walio chini yake badala ya kufanya hivyo kimaandishi au ofisini.Nilieleza kwamba japo dhamira ya Lowassa kukosoa utendaji wa subordinates ni njema,njia anazotumia sio mwafaka.Nilihoji kiongozi angejisikiaje iwapo Bosi wake,JK,akitokea kumkosoa hadharani badala ya kufanya hivyo faraghani.Nilipoandika makala hiyo,sikujua kuwa kuna siku,Lowassa atakumbana na fedheha ileile aliyokuwa akiwapatia ma-DC,RAS,Katibu Kata,nk kwa kuwaumbua hadharani (pengine kwa kujitafutia tu umaarufu wa kisiasa).Leo siku hiyo imetimia.Siku chache baada ya makala hiyo kuchapishwa,Mwandishi wa Habari wa Lowassa,aliandika makala kupinga hoja zangu,kabla ya kunitumia barua-pepe ya shutuma na hatimaye aliweka comments kwenye blog hii.Contents za makala,barua-pepe na comments za muungwana huyo zilikuwa na ujumbe unaolingana,ambapo pamoja na mambo mengine alipingana na hoja zangu huku akishutumu kwamba sie wanafunzi tulio nje tukisomeshwa kwa kodi za masikini hatupaswi kukosoa mambo tusiyoyajua (BONYEZA HAPA KUSOMA COMMENTS HIZO.)Nami nimjibu kwa barua-pepe kusisitiza kwamba nilichoandika kilikuwa sahihi,na imani yangu kwamba utetezi wake kwa Lowassa ilikuwa sehemu tu ya utekelezaji wa majukumu yake ya kazi (SOMA BARUA-PEPE HIYO KWA KUBONYEZA HAPA)
Makala yangu ndani ya toleo la wiki hii la gazeti la Raia Mwema iliandaliwa kabla ya "kimuhemuhe" kilichoanza leo huko Bungeni.Kwa kifupi,makala hiyo inaelezea namna siasa inavyoboa (au ni wanasiasa ndio wanaoboa?) na kutoa mfano wa namna baadhi ya wahafidhina katika chama cha Republicans "wanavyotiana vidole kwenye macho" kufuatia mwenendo mzuri wa harakati za Seneta John McCain kuingia White House kwa tiketi ya chama hicho.Pamoja na makala nyingine zilizokwenda shule ndani ya gazeti hilo,bingirika na makala yangu hiyo kwa KUBONYEZA HAPA.
Makala yangu hii ilitoka katika toleo la jana la gazeti la MtanzaniaSubscribe to our newsletter to get the latest updates to your inbox. ;-)
Your email address is safe with us!

Makala yangu hii ilitoka katika toleo la jana la gazeti la Mtanzania