
Pamoja na mambo mengine,makala yangu katika toleo la wiki hii la gazeti la
Raia Mwema inatoa changamoto kwa vyombo vya habari vya Tanzania kutumia ipasavyo teknolojia ya habari kwa kuwezesha habari zao kupatikana mtandaoni.Pia nimegusia kwa kifupi
"tangazo" la Balozi Ali Karume kuhusu dhamira yake ya kugombea urais wa Zanzibar mwaka 2010.Vilevile nimetumia sehemu kubwa kuelezea namna
ziara ya Rais Bush nchini Tanzania inavyoweza kusaidia mapambano dhidi ya ufisadi,hasa kama "tukimwaminisha" kuwa fedha zinazoibiwa na mafisadi hao zinaweza kuishia mikononi mwa akina
Osama bin Laden (
well,pengine mafisadi hawana uhusiano na magaidi wa kimataifa lakini wengi tunajua kwamba neno UGAIDI likihusishwa na kitu chochote kile/mtu yeyote yule lazima itamsukuma
Bush kufanya kitu flani).Bingirika na makala hiyo na nyinginezo zilizokwenda shule kwenye gazeti mwanana la
Raia Mwema kwa
KUBONYEZA HAPA
Posted in: ALI KARUME,GEORGE W BUSH,OSAMA BIN LADEN,RAIA MWEMA,TANZANIA,UFISADI,UGAIDI
Email This
BlogThis!
Share to Facebook
No comments :
Post a Comment