MKURUGENZI wa Kituo cha Uwekezaji nchini (TIC), Emmanuel ole Naiko, amesema neno ufisadi linawatisha wawekezaji, hivyo kuwataka wananchi kulitumia kwa umakini huku
wakiweka uzalendo mbele.
Alisema wakati taratibu za kupambana na rushwa zikiendelea, kipaumbele kielekezwe kwenye uchumi na maendeleo kwa ujumla ili kulikwamua taifa, kwani kiwango cha rushwa kilichopo si kama kilichopo katika nchi zilizoendelea.
Naiko alisema hayo jana katika mahojiano maalumu na Tanzania Daima, yaliyofanyika katika ofisi za TIC, jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi huyo alisema hakuna shaka kwamba rushwa na uwekezaji, haviendi pamoja lakini ni vema suala hili likachukuliwa kwa umakini na kutanguliza uzalendo kwa masilahi ya taifa.
“Tunatakiwa tuwe na uzalendo pale penye sifa mbaya, tulichukulie kwa umakini ili tusiendelee kulijengea sifa mbaya taifa letu. Tuziache taratibu na sheria zetu zifanye kazi, ikiwemo kuwapeleka mahakamani watuhumiwa,” alisema.
Alisema Tanzania haiongozi kwa rushwa lakini inaonekana hivyo kutokana na msimamo wa serikali kuweka wazi masuala ya rushwa. Akitolea mfano wa meya aliyeuza kiti cha useneta huko Illinois, nchini Marekani, Ole Naiko alisema hali hiyo inaashiria ni kwa jinsi gani kulivyo na rushwa katika nchi tajiri kuliko zile maskini.
“Sisi tuna rushwa ndogo ndogo, hatuwezi kuongoza kwa rushwa, nchi tajiri ndizo zinazoongoza kwa rushwa. Kwanza tuna taasisi za kupambana na rushwa na tunayaweka haya masuala wazi, wenyewe kamwe hawawezi, kwani hawataki nchi zao
zionekane mbaya,” alisisitiza. Kutokana na hali hiyo, Mkurugenzi aliwataka Watanzania kulifikiria taifa lao wakati likipambana na rushwa na kusisitiza kuwa wananchi wajadili jinsi ya kuliletea taifa maendeleo.
Akizungumzia mafanikio ya mkutano wa Sullivan uliofanyika mwaka jana, alisema huandaliwa kwa lengo la kuwaunganisha Wamarekani na Waafrika katika kujadili mustakabali wa jinsi ya kuondokana na hali ya umaskini inayowakabili.
Pamoja na hilo, alikiri kwamba mafanikio yameonekana hasa kwa wawekezaji wa Kimarekani, kwani mkutano huo umeifanya Marekani itoke nafasi ya nane hadi ya nne kwa uwekezaji nchini, ikifuatiwa na nchi za Uingereza, Afrika Kusini na Kenya.
Kuhusu safari za Rais Jakaya Kikwete nchini Marekani, Naiko alisema zimewawezesha Wamarekani kuifahamu vema Tanzania, hivyo kuvutika kuwekeza zaidi. Alisema kwa sasa kituo chake kina mpango mahususi wa kutumia balozi zake katika kuitangaza Tanzania, ikiwa ni pamoja na kuweka balozi zake katika nchi zenye uwezo wa kuwekeza nchini.CHANZO: Tanzania Daima
MASLAHI YA TAIFA YATALINDWA TU ENDAPO KELELE DHIDI YA MAFISADI ZITAENDELEA KWA NGUVU KUBWA NA KUWASHIRIKISHA WATU KAMA OLE NAIKO NA WALA SIO KWA KUONGEA CHINICHINI KWA KUHOFIA KUWATISHA WAWEKEZAJI.HIVI MAFISADI WAKISHAIFILISI TANZANIA HAO WAWEKEZAJI WATAKUJA KUWEKEZA KWENYE NINI?
WAUMINI wa dini ya kiislam wamepinga oparesheni sangara
inayoendeshwa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kwa madai kuws
chama hicho na operesheni hiyo, haina manufaa kwa uisalam kwa kuwa imejaa
ukabila, ubinafisi na udini
Wakizungumza kwa nyakati tofauti kwenye
kongamano la kiisilamu, lililofanyika jana jijini Dar es Salaam, walisema
oparasheni Sangara imekuwa ikimchafua rais Jakaya Kikwete bila sababu licha ya
mambo mengi mazuri, aliyoyafanya kwa taifa.
Shekhe Saidi Mwaipopo aliwataka
waisalamu kutambua kuwa chama hicho, hakina msaada wowote wa maendeleo ya
uislamu kutokana na chama hicho kujaa ukabila udini na ubinafisi.
"Napenda
waislamu muelewe kuwa chama cha Chadema hakina msaada wowote juu ya uislamu na
kimekumbatia udini, ukabila na ubinafisi kutokana na sababu hiyo, tutatembea
nchi nzima kuwaeleza wanachi ukweli wa jambo hili na kuwataka wasikiunge mkono
chama hicho,"alisema Mwaipopo...ENDELEA
Visit msnbc.com for Breaking News, World News, and News about the Economy
Subscribe to our newsletter to get the latest updates to your inbox. ;-)
Your email address is safe with us!