Subscribe to our newsletter to get the latest updates to your inbox. ;-)
Your email address is safe with us!
Kuhusu ziara za JK nchi za nje, napenda kusema kuwa mkurugenzi wa kituo cha uwekezaji Tanzania (Tanzania Investment Center), Mheshimiwa Ole Naiko, amesema na kurudia kuwa ziara za JK nchi za nje zimeleta faida nchini, kwa upande wa uwekezaji na biashara. Kwa mfano, miezi kadhaa iliyopita aliongelea jinsi kiwango cha uwekezaji kutoka Marekani ulivyopanda mara dufu kutokana na ziara za JK. Hivi karibuni, Ole Naiko ameongelea manufaa ya ziara ya JK na wafanyabiashara wa Tanzania huko Uturuki. Ole Naiko amesema wazi kuwa wanaobeza ziara za JK nchi za nje hawana takwimu, na hawaitakii nchi mema. Maneno yake hayo yako huko mtandaoni pia.
Mimi si mtaalam wa masuala hayo, bali nileta tu hii taarifa kuhusu kauli za mkurugenzi wa TIC.
Profesa,laiti takwimu tunazopewa na watawala wetu zingekuwa sio tu za kuaminika bali pia zinaendana na hali halisi "mtaani" basi yayumkinika kusema kuwa leo hii tusingekuwa "taifa la dunia ya tatu".Ni dhahiri kuwa laiti ziara hizo zingekuwa zimeleta ufanisi kiasi anachotuaminisha Mheshimiwa Ole Naiko basi nchi wahisani wasingepunguza sehemu ya msaada wao kwa kigezo cha "uzembe" na urasimu kwenye eneo hilohilo la uwekezaji.Na huyo Ole Naiko na TIC yake ingekuwa inawajibika ipasavyo tusingelazimika kuwalipa Wabrazili mabilioni ya shilingi kwa minajili ya "kuitangaza Tanzania" kwa dakika 90.
Takwimu nyingi zimekuwa za kuleta matumaini sana,na majuzi Mkulo ametuambia kuwa uchumi unakua huku akitoa takwimu za kupendeza.MKUKUTA,MKURABITA,MWEMKWA,nk nk zinafanya vizuri in terms of takwimu,lakini hali ya Watanzania inazidi kuwa duni.
Hivi wewe Profesa Mbele unategemea huyo Naiko anaweza kumkosoa JK...Hivi unataka nini kiongelewe ndiyo ufahamu hiyo serikali ya JK ni ya ubabaishaji...wala rushwa wote ambao ushahidi umetolowa na magazeti makini kabisa kama the Guardian and na taasisi SFO..na kesi zingine nyingi na hizo zote zipo ndani ya uwezo serikali ya JK anashindwa kuchukua hatua zozote kama Rais wa Jamhuri...na kushindwa kwake kuchukua hizo hatua ndiyo inaonesha wazi kuwa hao Mafisadi na wala Rushwa ndiyo maswahiba wake au wanaisa wenzake. Hivyo tunapenda uwe muwazi kama maandishi ya ripoti ndiyo maendeleo ya Tanzania ingekuwa mbali sana kwenye kuondoa umaskini na hata wewe Profesa Mbele ungekuwa unafundisha vyuo vya Tanzania...Tunaomba acaha kutetea uzembe wa serakali hii...tusiposema na kukosoa uozo wa serikali hii kama wewe Profesa hatutafika popote.....Big up Dr Chahali kwa mawazo yakinifu yenye dira halisi ya kuleta uwazi bila kificho katika madudu ya serikali ya JK.
Mimi ni mjumbe. Nimeleta msimamo wa TIC. Nashangaa kuwa kwa kufanya hivyo, nasemwa kuwa ni mtetezi wa serikali ya JK na kadhalika.
Ukweli kama mimi ni mtetezi wa serikali ya JK au la ummejaa katika kitabu changu kuhusu masuala ya siasa na jamii ya Tanzania enzi hizi za JK. Bofya hapa.
Nikisema kuwa wa-Tanzania watasoma kitabu changu nitakuwa nawapa sifa ambayo hawastahili. Ni wachache sana wanaosoma vitabu.
Nimeshatamka tena na tena, kwenye blogu yangu na blogu za wengine, kuwa wa-Tanzania ni wazembe inapofika kwenye suala la kununua au kusoma vitabu. Wanaona ni kero, labda viwe vitabu vya udaku.
Kuhusu ufisadi ni kuwa wa-Tanzania wenyewe wanaulea na kuuenzi ufisadi, kuanzia vijijini hadi mijini, shuleni, viwandani, hospitalini, maofisini, na kadhalika. Nimeshatamka kuwa wa-Tanzanai wanapolalamikia ufisadi miongoni mwa vigogo serikalini au kwenye mashirika wanafanya usanii. Bofya hapa.
Huwa sioni sababu ya kujibizana na "anonymous." Sijui kama ni woga au usanii unaowafanya watu wajifiche kwenye malumbano. Bofya hapa.
"Anonymous" wa hapo juu analeta mpya kwa jinsi anavyomalizia ujumbe wake kwa kupigia debe "uwazi bila kificho" wakati yeye mwenyewe yuko mafichoni. Ndio usanii ninaokataa mimi huo.
Kwa Profesa Mbele,
Kuwa mjumbe wa TIC ni jambo jema kufanya hivyo lakini taarifa zilizopo tuu kwenye maandishi na siyo kielelezo katika maisha halisi ya mtanzania. Mimi ni Mtanzania niliyopo hapa Tanzania. Tunatambua kuwa huko mlipo ninyi watanzania wenzetu mliyopo huko ughaibuni mnaona na kushuhudia mengi katika maarifa na matukio ya uchumi duniani.
Hivi tunapozungumzia utalii tunalenga mataifa ya makubwa ya magharibi na kwa sababu hiyo. JK anatumia nafasi kwenda nchi za magharibi anakosema yeye anatangaza utalii wakati watu wenyewe anaowatangazia wanamatatizo ya uchumi!!!!!!.Safari za nje Kama hapa ilivyofafanuliwa hapa na DR Chahali...Je huyo waziri wa mambo nje anafanya nini na balozi Tanzania anafanya nini? This is very strange to be defended from you Prof. Mbele...I can’t understand you at all means to be like this!!!!!
Sasa hizo takwimu za kusema utalii kuongezeka zinatoka wapi!? Ni ukweli kwamba watu wa magharibi watu makini sana linapokuja suala la matumizi ya pesa wanapokuwa katika kipindi kigumu kwenye uchumi wao...Sasa hao watalii unaosema wametoka wapi!!!!????
Iwapo wewe ungekuwa makini na upendo na watanzania husinge weka utaratibu wa ununuajia wa kitabu chako kwa asilimia mia moja kutegemea teknolojia ambayo sisi watanzania tupo chini asilimia moja wanaojua jinsi ya kutumia computer mbaya zaidi kuna uhalifu mkubwa katika intanet ambayo unahitaji elimu na maarifa kuutambua huo.
Sasa unaposema tununue kwa pesa ipi tuliyokuwa nayo. Na pesa zote wamechukua maswahiba wake huyo unayeshindwa kumkosoa waziwazi mpaka sisi tununua haya mawazo yako. Sasa tofauti yako wewe na hao mafisadi ni ipi!??
Hizo habari za udaku zinaandikwa na vyanzo vipi vya habari....iwapo kama ni magazeti ni mangapi kwa idadi...Wewe unafikiri magazeti yote ya udaku yana-nafasi sawa katika jamii hii ya kitanzania. Sisi ndiyo tunamatatizo idadi yetu ni milioni arobaini.
Nategemea wewe unaangalia kundi la watu milioni nne ndiyo watanzania wote. Sisi ni watanzania milioni arobaini wenye sifa kuishi kwa siku chini ya dola moja kwa siku, hivyo basi kati yetu kutumia hiyo £10 au nane kununua kitabu chako ni sawa na kipato chetu cha miezi mitatu. Sasa tukae bila kula, kuoga, kuandaa mashmab yetu, kununua kalamu kwa ajili ya familia zetu kwenda shule, bila matibabu ndiyo tutaweza kununua kitabu chako.
Maneno yako yanatukumbusha msemo wa Kiswahili unaosema aliyeshiba hamfahamu aliyelala njaa. Na hii inathibitisha mara nyingi katika maoni yako kushindwa kuikosoa serikali ya JK kuwa serikali hii ni zuga.
Inaendelea kwa ajili ya Profsa Mbele,
Nikukumbushe tuu mwalimu ama kiongozi yeyote ni kielelezo cha jamii kama wewe uliyemkufunzi wa chuo kikuu huko unakoishi na kuja kututembelea hapa kwa muda mfupi na kuondoka kwenda peponi na kutuacha sisi hapa motoni na baadae kutoa hayo maoni ya kuogofya(shocking).
Hivyo basi iwapo wewe ni kiongozi katika jamii basi ni rahisi sana kuisaidia jamii hii ama kuingamiza. Na hiyo dhana inayotumika na CCM na serikali ya Kikwete kuiangaamiza jamii yetu na wewe Profesa Mbele ukishirkia kwa kujiita Mjumbe wa TIC.
Kukuthibitishia hayo kashfa ya rada, kagoda na hao dada zake, Richmond na dada zake, migodi kuuzwa, mashirika ya umma, Menejiment ya kuingoza TANESCO iliyoingizwa madarakani kwa mtutu kwa Baraka za Kikwete wahusika wake wangekuwa jela hivi sasa na pia kufilisiwa ndiyo ungesema kwamba watanzania wote katika ngazi zote wanaweza kuwa hai kupambana kuondoa ufisadi hivi sasa haiwezekana kwa sababu kuanzia ngazi juu(Rais angalia kauli zake kutoka ughaibuni blog) kabisa yenye uwezo na mamlaka kupambana na Rushwa na ufisadi ndiyo wanabariki huu uhalifu. Tunatambua kwamba wewe ni miongoni watu walilelewa na CCM na pia hata kusomeshwa bila kukopeshwa mpaka elimu ya chuo kikuu hivyo unaona dhambi kama vile kuikosoa serikali ya CCM ni sawa na kuhua mtu vile.
Kujificha kwangu inatokana na watu kama wewe profesa Mbele..baada kuongelea suala la muhimu unaleta masihara katika mtoa maoni sababu kuwa na status of an anonymous...these are just options available from Dr Chahali Blog kwa sisi tunaogopa kufahamika kwa mtu kama wewe. Kimsingi naweza kukuita wakala wao hao tunaotaka haki itendeke ili tuendeshe Taifa letu tunalolipenda.
Nategema utakuwa umeelewa wewe mtu wa namna gani ili uweze kujitafakari iwapo unayo nia ya kufanya hivyo kuwa nje ya TANZANIA incorrupt network.

Kukuthibitishia hayo kashfa ya rada, kagoda na hao dada zake, Richmond na dada zake, migodi kuuzwa, mashirika ya umma, Menejiment ya kuingoza TANESCO iliyoingizwa madarakani kwa mtutu kwa Baraka za Kikwete wahusika wake wangekuwa jela hivi sasa na pia kufilisiwa ndiyo ungesema kwamba watanzania wote katika ngazi zote wanaweza kuwa hai kupambana kuondoa ufisadi hivi sasa haiwezekana kwa sababu kuanzia ngazi juu(Rais soma kauli zake kutoka ughaibuni blog) kabisa yenye uwezo na mamlaka kupambana na Rushwa na ufisadi ndiyo wanabariki huu uhalifu. Tunatambua kwamba wewe ni miongoni watu walilelewa na CCM na pia hata kusomeshwa bila kukopeshwa mpaka elimu ya chuo kikuu hivyo unaona dhambi kama vile kuikosoa serikali ya CCM ni sawa na kuhua mtu vile.

Big up Dr Chahali for showing us your nationalism spirit.
Profesa,binafsi sina tatizo na wewe mwalimu wangu kutukumbusha ujumbe wa TIC lakini tatizo langu lipo kwa hao TIC wenyewe na utendaji wao kwa ujumla.
Japo naafikiana nawe Profesa kuwa kusoma machapisho ni tatizo miongoni mwa Watanzania wengi lakini kwa upande mwingine tatizo ni kilichomo katika machapisho husika.Hivi katika mazingira ya sasa ambapo Watanzania wengi wako hoi kiuchumi,haiyumkiniki kubashiri kuwa machapisho yenye kuelemea zaidi kwenye takwimu pasipo kujali hali halisi yatapuuzwa?Nachomaanisha hapa ni tabia iliyojengeka miongoni mwa waandishi wengi kuandika kama “watazamaji” au “waangalizi” walio nje ya jamii wanayoilenga badala ya kuwa sehemu ya jamii hiyo.Ni dhahiri,kwa mfano,kitabu kinachodai kuwa uwekezaji umeinufaisha Tanzania kitaonekana kama “kamusi ya matusi” kwa “watu wa kawaida mtaani”.
Halafu kuna tatizo la lugha inayotumika katika mengi ya machapisho hayo. Kuna tofauti kati ya mhadhara kwenye warsha au darasa la wanafunzi wa chuo kikuu..Pengine hicho kinachochea baadhi ya watu kupendelea zaidi machapisho ya udaku kuliko “hayo ya maana” kwani hawaoni umuhimu wa kupoteza muda kusoma kitu kisichoeleweka au kinachoelezea mambo tofauti na uhalisia (kana kwamba mwandishi anaishi sayari tofauti na wasomaji wake).
Kuhusu wanaotoa mawazo yao kama “anonymous” (kama huyo mchangiaji hapo juu) binafsi sina tatizo sana kwa vile la muhimu zaidi kwangu ni uzito na mantiki ya hoja zao na si majina yao.Kadhalika,naheshimu haki za kibinadamu za watoa maoni wanaoamua kutotumia majina yao wanapotoa maoni yao.Ni kama katika filamu ambapo wahusika wengi hutumia majina bandia na kinachoifanya filamu ivutie sio jina la mhusika bali ubora (na pengine ujumbe) wa filamu husika.Na hata baadhi ya waandishi maarufu wamekuwa wakitumia majina bandia (kwa mfano James Hadley Chase) lakini haikuzuwia machapisho yao kuwa world bestsellers.Hata hivyo,binafsi napenda kutumia jina langu halisi kila napoweka comments mahala flani.Kwanini?Kubwa zaidi ni uamuzi wangu tu.
Japo naafikiana nawe Profesa kuwa Watanzania hawawezi kukwepa kabisa mchango wao katika kushamiri kwa ufisadi,natofautiana nawe kidogo kwa sababu hii: Kwa uelewa wangu mdogo,mahusiano mbalimbali katika jamii yanategemea sana umiliki wa nyenzo za uzalishaji mali na mahusiano ya nguvu za uzalishaji mali (power relations).Ni rahisi kulilaumu tabaka tawaliwa kwa “kuzembea” kuliwajibisha tabaka tawala iwapo anayelaumu haangalii namna tabaka tawala linavyojizatiti kudumisha nafasi yake.Kwahiyo,ni rahisi kuwalaumu walalahoi “wanavyolea ufisadi” iwapo tunafumbia macho mazingira yaliyotengenezwa na tabaka tawala dhidi ya “wanaopinga ufisadi”.
Hivi katika mazingira ya sasa ambapo ni rahisi zaidi kumweka madarakani mbunge (kwa njia halali za kidemokrasia) kuliko kumtoa madarakani hata kama amebainika kupata ubunge huo kwa kugushi sifa zake za kitaaluma (rejea suala la Mheshimiwa Chitalo),au katika mazingira ya sasa ambapo rais ni mithili ya mungu-mtu kutokana na nguvu lukuki alizolimbikiziwa (na kwa bahati mbaya au makusudi zimeishia kwenye kutuambia tu “wala rushwa wanajulikana,nawapa muda wa kujirekebisha...”),mtu wa kawaida mtaani afanyeje?Na je katika mazingira haya ambapo mara nyingi mksanyiko “halali” ni wa kusikiliza hotuba za viongozi wa chama tawala,na madamano “halali” ni ya kupongeza kauli flani za watawala wetu na sio kupingana nazo,mwananchi wa kawaida anapata wapi nafasi ya kuwawajibisha watawala?Na hapo tunaweka kando lawama tunazopaswa kutumiwa sie tuliobahatika “kuona ndani ya darasa”-au tabaka la kati kwa ujumla pamoja na civil society-kwa namna tunavyojiweka karibu zaidi na tabaka tawala na kulitelekeza tabaka tawaliwa.
Nyerere alitufundisha kuwa ili tuendelee tunahitaji watu,ardhi,siasa safi na uongozi bora,na kwa vile hakuna mtu anayependa kuwa fukara au kunyonywa,na pia ardhi tunayo ya “kumwaga”,kwa hakika kinachotukwamisha ni mapungufu katika siasa na uongozi,au kwa ufasaha zaidi, siasa za kifisadi na uongozi wa kizushi.
Kuhusu ziara za JK nchi za nje, napenda kusema kuwa mkurugenzi wa kituo cha uwekezaji Tanzania (Tanzania Investment Center), Mheshimiwa Ole Naiko, amesema na kurudia kuwa ziara za JK nchi za nje zimeleta faida nchini, kwa upande wa uwekezaji na biashara. Kwa mfano, miezi kadhaa iliyopita aliongelea jinsi kiwango cha uwekezaji kutoka Marekani ulivyopanda mara dufu kutokana na ziara za JK. Hivi karibuni, Ole Naiko ameongelea manufaa ya ziara ya JK na wafanyabiashara wa Tanzania huko Uturuki. Ole Naiko amesema wazi kuwa wanaobeza ziara za JK nchi za nje hawana takwimu, na hawaitakii nchi mema. Maneno yake hayo yako huko mtandaoni pia.
ReplyDeleteMimi si mtaalam wa masuala hayo, bali nileta tu hii taarifa kuhusu kauli za mkurugenzi wa TIC.
Profesa,laiti takwimu tunazopewa na watawala wetu zingekuwa sio tu za kuaminika bali pia zinaendana na hali halisi "mtaani" basi yayumkinika kusema kuwa leo hii tusingekuwa "taifa la dunia ya tatu".Ni dhahiri kuwa laiti ziara hizo zingekuwa zimeleta ufanisi kiasi anachotuaminisha Mheshimiwa Ole Naiko basi nchi wahisani wasingepunguza sehemu ya msaada wao kwa kigezo cha "uzembe" na urasimu kwenye eneo hilohilo la uwekezaji.Na huyo Ole Naiko na TIC yake ingekuwa inawajibika ipasavyo tusingelazimika kuwalipa Wabrazili mabilioni ya shilingi kwa minajili ya "kuitangaza Tanzania" kwa dakika 90.
ReplyDeleteTakwimu nyingi zimekuwa za kuleta matumaini sana,na majuzi Mkulo ametuambia kuwa uchumi unakua huku akitoa takwimu za kupendeza.MKUKUTA,MKURABITA,MWEMKWA,nk nk zinafanya vizuri in terms of takwimu,lakini hali ya Watanzania inazidi kuwa duni.
Hivi wewe Profesa Mbele unategemea huyo Naiko anaweza kumkosoa JK...Hivi unataka nini kiongelewe ndiyo ufahamu hiyo serikali ya JK ni ya ubabaishaji...wala rushwa wote ambao ushahidi umetolowa na magazeti makini kabisa kama the Guardian and na taasisi SFO..na kesi zingine nyingi na hizo zote zipo ndani ya uwezo serikali ya JK anashindwa kuchukua hatua zozote kama Rais wa Jamhuri...na kushindwa kwake kuchukua hizo hatua ndiyo inaonesha wazi kuwa hao Mafisadi na wala Rushwa ndiyo maswahiba wake au wanaisa wenzake. Hivyo tunapenda uwe muwazi kama maandishi ya ripoti ndiyo maendeleo ya Tanzania ingekuwa mbali sana kwenye kuondoa umaskini na hata wewe Profesa Mbele ungekuwa unafundisha vyuo vya Tanzania...Tunaomba acaha kutetea uzembe wa serakali hii...tusiposema na kukosoa uozo wa serikali hii kama wewe Profesa hatutafika popote.....Big up Dr Chahali kwa mawazo yakinifu yenye dira halisi ya kuleta uwazi bila kificho katika madudu ya serikali ya JK.
ReplyDeleteMimi ni mjumbe. Nimeleta msimamo wa TIC. Nashangaa kuwa kwa kufanya hivyo, nasemwa kuwa ni mtetezi wa serikali ya JK na kadhalika.
ReplyDeleteUkweli kama mimi ni mtetezi wa serikali ya JK au la ummejaa katika kitabu changu kuhusu masuala ya siasa na jamii ya Tanzania enzi hizi za JK. Bofya hapa.
Nikisema kuwa wa-Tanzania watasoma kitabu changu nitakuwa nawapa sifa ambayo hawastahili. Ni wachache sana wanaosoma vitabu.
Nimeshatamka tena na tena, kwenye blogu yangu na blogu za wengine, kuwa wa-Tanzania ni wazembe inapofika kwenye suala la kununua au kusoma vitabu. Wanaona ni kero, labda viwe vitabu vya udaku.
Kuhusu ufisadi ni kuwa wa-Tanzania wenyewe wanaulea na kuuenzi ufisadi, kuanzia vijijini hadi mijini, shuleni, viwandani, hospitalini, maofisini, na kadhalika. Nimeshatamka kuwa wa-Tanzanai wanapolalamikia ufisadi miongoni mwa vigogo serikalini au kwenye mashirika wanafanya usanii. Bofya hapa.
Huwa sioni sababu ya kujibizana na "anonymous." Sijui kama ni woga au usanii unaowafanya watu wajifiche kwenye malumbano. Bofya hapa.
"Anonymous" wa hapo juu analeta mpya kwa jinsi anavyomalizia ujumbe wake kwa kupigia debe "uwazi bila kificho" wakati yeye mwenyewe yuko mafichoni. Ndio usanii ninaokataa mimi huo.
Kwa Profesa Mbele,
ReplyDeleteKuwa mjumbe wa TIC ni jambo jema kufanya hivyo lakini taarifa zilizopo tuu kwenye maandishi na siyo kielelezo katika maisha halisi ya mtanzania. Mimi ni Mtanzania niliyopo hapa Tanzania. Tunatambua kuwa huko mlipo ninyi watanzania wenzetu mliyopo huko ughaibuni mnaona na kushuhudia mengi katika maarifa na matukio ya uchumi duniani.
Hivi tunapozungumzia utalii tunalenga mataifa ya makubwa ya magharibi na kwa sababu hiyo. JK anatumia nafasi kwenda nchi za magharibi anakosema yeye anatangaza utalii wakati watu wenyewe anaowatangazia wanamatatizo ya uchumi!!!!!!.Safari za nje Kama hapa ilivyofafanuliwa hapa na DR Chahali...Je huyo waziri wa mambo nje anafanya nini na balozi Tanzania anafanya nini? This is very strange to be defended from you Prof. Mbele...I can’t understand you at all means to be like this!!!!!
Sasa hizo takwimu za kusema utalii kuongezeka zinatoka wapi!? Ni ukweli kwamba watu wa magharibi watu makini sana linapokuja suala la matumizi ya pesa wanapokuwa katika kipindi kigumu kwenye uchumi wao...Sasa hao watalii unaosema wametoka wapi!!!!????
Iwapo wewe ungekuwa makini na upendo na watanzania husinge weka utaratibu wa ununuajia wa kitabu chako kwa asilimia mia moja kutegemea teknolojia ambayo sisi watanzania tupo chini asilimia moja wanaojua jinsi ya kutumia computer mbaya zaidi kuna uhalifu mkubwa katika intanet ambayo unahitaji elimu na maarifa kuutambua huo.
Sasa unaposema tununue kwa pesa ipi tuliyokuwa nayo. Na pesa zote wamechukua maswahiba wake huyo unayeshindwa kumkosoa waziwazi mpaka sisi tununua haya mawazo yako. Sasa tofauti yako wewe na hao mafisadi ni ipi!??
Hizo habari za udaku zinaandikwa na vyanzo vipi vya habari....iwapo kama ni magazeti ni mangapi kwa idadi...Wewe unafikiri magazeti yote ya udaku yana-nafasi sawa katika jamii hii ya kitanzania. Sisi ndiyo tunamatatizo idadi yetu ni milioni arobaini.
Nategemea wewe unaangalia kundi la watu milioni nne ndiyo watanzania wote. Sisi ni watanzania milioni arobaini wenye sifa kuishi kwa siku chini ya dola moja kwa siku, hivyo basi kati yetu kutumia hiyo £10 au nane kununua kitabu chako ni sawa na kipato chetu cha miezi mitatu. Sasa tukae bila kula, kuoga, kuandaa mashmab yetu, kununua kalamu kwa ajili ya familia zetu kwenda shule, bila matibabu ndiyo tutaweza kununua kitabu chako.
Maneno yako yanatukumbusha msemo wa Kiswahili unaosema aliyeshiba hamfahamu aliyelala njaa. Na hii inathibitisha mara nyingi katika maoni yako kushindwa kuikosoa serikali ya JK kuwa serikali hii ni zuga.
Inaendelea kwa ajili ya Profsa Mbele,
ReplyDeleteNikukumbushe tuu mwalimu ama kiongozi yeyote ni kielelezo cha jamii kama wewe uliyemkufunzi wa chuo kikuu huko unakoishi na kuja kututembelea hapa kwa muda mfupi na kuondoka kwenda peponi na kutuacha sisi hapa motoni na baadae kutoa hayo maoni ya kuogofya(shocking).
Hivyo basi iwapo wewe ni kiongozi katika jamii basi ni rahisi sana kuisaidia jamii hii ama kuingamiza. Na hiyo dhana inayotumika na CCM na serikali ya Kikwete kuiangaamiza jamii yetu na wewe Profesa Mbele ukishirkia kwa kujiita Mjumbe wa TIC.
Kukuthibitishia hayo kashfa ya rada, kagoda na hao dada zake, Richmond na dada zake, migodi kuuzwa, mashirika ya umma, Menejiment ya kuingoza TANESCO iliyoingizwa madarakani kwa mtutu kwa Baraka za Kikwete wahusika wake wangekuwa jela hivi sasa na pia kufilisiwa ndiyo ungesema kwamba watanzania wote katika ngazi zote wanaweza kuwa hai kupambana kuondoa ufisadi hivi sasa haiwezekana kwa sababu kuanzia ngazi juu(Rais angalia kauli zake kutoka ughaibuni blog) kabisa yenye uwezo na mamlaka kupambana na Rushwa na ufisadi ndiyo wanabariki huu uhalifu. Tunatambua kwamba wewe ni miongoni watu walilelewa na CCM na pia hata kusomeshwa bila kukopeshwa mpaka elimu ya chuo kikuu hivyo unaona dhambi kama vile kuikosoa serikali ya CCM ni sawa na kuhua mtu vile.
Kujificha kwangu inatokana na watu kama wewe profesa Mbele..baada kuongelea suala la muhimu unaleta masihara katika mtoa maoni sababu kuwa na status of an anonymous...these are just options available from Dr Chahali Blog kwa sisi tunaogopa kufahamika kwa mtu kama wewe. Kimsingi naweza kukuita wakala wao hao tunaotaka haki itendeke ili tuendeshe Taifa letu tunalolipenda.
Nategema utakuwa umeelewa wewe mtu wa namna gani ili uweze kujitafakari iwapo unayo nia ya kufanya hivyo kuwa nje ya TANZANIA incorrupt network.
Nikukumbushe tuu mwalimu ama kiongozi yeyote ni kielelezo cha jamii kama wewe uliyemkufunzi wa chuo kikuu huko unakoishi na kuja kututembelea hapa kwa muda mfupi na kuondoka kwenda peponi na kutuacha sisi hapa motoni na baadae kutoa hayo maoni ya kuogofya(shocking).
Hivyo basi iwapo wewe ni kiongozi katika jamii basi ni rahisi sana kuisaidia jamii hii ama kuingamiza. Na hiyo dhana inayotumika na CCM na serikali ya Kikwete kuiangaamiza jamii yetu na wewe Profesa Mbele ukishirkia kwa kujiita Mjumbe wa TIC.
Kukuthibitishia hayo kashfa ya rada, kagoda na hao dada zake, Richmond na dada zake, migodi kuuzwa, mashirika ya umma, Menejiment ya kuingoza TANESCO iliyoingizwa madarakani kwa mtutu kwa Baraka za Kikwete wahusika wake wangekuwa jela hivi sasa na pia kufilisiwa ndiyo ungesema kwamba watanzania wote katika ngazi zote wanaweza kuwa hai kupambana kuondoa ufisadi hivi sasa haiwezekana kwa sababu kuanzia ngazi juu(Rais soma kauli zake kutoka ughaibuni blog) kabisa yenye uwezo na mamlaka kupambana na Rushwa na ufisadi ndiyo wanabariki huu uhalifu. Tunatambua kwamba wewe ni miongoni watu walilelewa na CCM na pia hata kusomeshwa bila kukopeshwa mpaka elimu ya chuo kikuu hivyo unaona dhambi kama vile kuikosoa serikali ya CCM ni sawa na kuhua mtu vile.
Kujificha kwangu inatokana na watu kama wewe profesa Mbele..baada kuongelea suala la muhimu unaleta masihara katika mtoa maoni sababu kuwa na status of an anonymous...these are just options available from Dr Chahali Blog kwa sisi tunaogopa kufahamika kwa mtu kama wewe. Kimsingi naweza kukuita wakala wao hao tunaotaka haki itendeke ili tuendeshe Taifa letu tunalolipenda.
Nategema utakuwa umeelewa wewe mtu wa namna gani ili uweze kujitafakari iwapo unayo nia ya kufanya hivyo kuwa nje ya TANZANIA incorrupt network.
Big up Dr Chahali for showing us your nationalism spirit.
Profesa,binafsi sina tatizo na wewe mwalimu wangu kutukumbusha ujumbe wa TIC lakini tatizo langu lipo kwa hao TIC wenyewe na utendaji wao kwa ujumla.
ReplyDeleteJapo naafikiana nawe Profesa kuwa kusoma machapisho ni tatizo miongoni mwa Watanzania wengi lakini kwa upande mwingine tatizo ni kilichomo katika machapisho husika.Hivi katika mazingira ya sasa ambapo Watanzania wengi wako hoi kiuchumi,haiyumkiniki kubashiri kuwa machapisho yenye kuelemea zaidi kwenye takwimu pasipo kujali hali halisi yatapuuzwa?Nachomaanisha hapa ni tabia iliyojengeka miongoni mwa waandishi wengi kuandika kama “watazamaji” au “waangalizi” walio nje ya jamii wanayoilenga badala ya kuwa sehemu ya jamii hiyo.Ni dhahiri,kwa mfano,kitabu kinachodai kuwa uwekezaji umeinufaisha Tanzania kitaonekana kama “kamusi ya matusi” kwa “watu wa kawaida mtaani”.