Featured Posts

Thursday, October 14, 2010

Mafanikio ya JK: Maisha Bora kwa Wastaafu wa Afrika Mashariki Yamewezekana (PICHA)

Wastaafu wa iliyokuwa Jumuiya ya Afrika Mashariki wakiwa wamejilaza tayari 'kusulubiwa na gari la upupu' la FFU.Kosa lao ni kufuatilia haki na stahili zao.

Wazee wetu wakipiga swala.Hivi Kikwete angewakalia kooni mafisadi wa Kagoda na wana-EPA wengine kisingepatikana japo kiasi cha mboga kuwatuliza wazee wetu hawa?

Katika moja ya hotuba zake Bungeni,Kikwete alikumbushia umuhimu wa haki za kinadamu za mafisadi.Vipi kuhusu haki za msingi za wazee hawa wasio na hatia?

Picha ya juu na chini: Wazee wetu wakijipoza kwa mlo baada ya awamu nyingine ya danadana za kupata haki zao.Natumaini wazee hawa wanafahamu nani ni kikwazo cha ufumbuzi wa tatizo lao.Haya ndio Maisha Bora aliyowaahidi Kikwete mwaka 2005.Na hiyo ndio Ari Mpya, Kasi Mpya na Nguvu Mpya ya kutatua kero zenu.Bado mnatafuta sababu za ziada za kumnyima kura?

Picha kwa Hisani ya MICHUZI JUNIOR (Jiachie).Maelezo ya picha ni yangu binafsi.

2 comments:

Anonymous said...

Kufanya kosa siyo kosa isipokuwa kuirudisha tena serikali ya CCM ndiyo kosa ambalo litawagharimu watanzania kwa maisha yetu yote.....Kwa kuwambusha tuu waonaamini mungu kwamba sisi watanzania tumepatiwa utashi na hekima na Mungu tuutumie kupata viongozi sahihi na siyo kama huyu JK na chama chake cha CCM

NN Mhango said...

Tusiilaumu CCM bali ujuha na upogo wa watu wetu. CCM kwa miongo mingi ilishaweka wazi iko kwa ajili ya mafisadi. Hivi kuinyima kura nako kunahitaji wafadhili au CCM?
Hawa jamaa wamezungushwa kwa miaka zaidi ya thelathini. Bado wana matumaini ilhali wengi wao wanazidi kupukutika? Wanataka waguswe wapi wastuke? Mbona pesa ya kuwalipa wezi na mafisadi waliotimuliwa madarakani kwa uchafu na ulafu wao ipo lakini siyo ya wachapakazi kama wao? Majibu ya maswali haya na mengine ni kuichagua CHADEMA iwakomboe na kuwapa haki zao na fidia juu.

Post a Comment

 
Design by Free WordPress Themes | Bloggerized by Lasantha - Premium Blogger Themes | Hot Sonakshi Sinha, Car Price in India