Featured Posts

Thursday, July 07, 2011

Baba Mzee Chahali Amepata Ajali Mbaya,Naomba Sala Zenu


Nasikitika kuwafahamisha kuwa baba mzazi Mzee Philemon Chahali amepata ajali mbaya asubuhi hii huko Ifakara.Amegongwa na pikipiki ambazo ndio usafiri mkuu wa huko.Kwa mujibu wa habari nilizonazo hadi muda huu,hali yake ni mbaya,ambapo licha ya kuvnjika mguu pia ameumia kichwani.Kibaya zaidi ni kwamba umri wake ni kwenye miaka ya 80 kwa hiyo mshtuko tu wa ajli unaweza kumwathiri sana.

Basi naomba kutumia fursa hii kuomba sala zenu.Sie Wakristo tunaamini kuwa wanapojumuka wengi kufanya sala basi Mungu naye anakuwepo.Natumaini kwa sala zenu na za familia yetu Mungu atamjalia baba apone na kurejea katika hali yake ya kawaida.

Natanguliza shukrani zangu za dhati.Asanteni 

8 comments:

SIMON KITURURU said...

Pole MKUU!

Na nakutakia upone haraka Mzee Philemon Chahali !

Swahili na Waswahili said...

Pole sana kaka Chahali na familia yote,Mungu yu pamoja na tuko pamoja katika maombi.

malkiory said...

Tuko pamoja kwenye maombezi ili baba yetu aweze kupona haraka.

La Princessa said...

In our prayers

EVARIST said...

Asanteni sana,Malkiory na La Princessa

Upepo Mwanana said...

tunamtakia kila la heri aweze kupona haraka

Nova Kambota Mwanaharakati said...

Rejea Maandiko matakatifu tunafundishwa kuwa hakuna linaloshindikana kwa Mungu hivyo wote kwa pamoja tunajongea mbele ya Mungu kwa unyenyekevu na kumwombea mzee wetu Philemon Chahali aweze kupona haraka na kuendelea na shughuli za maisha..AMEN!

Mwanasosholojia said...

Mungu mwenye nguvu, asiyeshindwa na lolote, kwa hakika atamponya mzee wetu Chahali na kumpa nguvu za kuendelea na majukumu yake. Tupo pamoja katika kumuombea mzee wetu

Post a Comment

 
Design by Free WordPress Themes | Bloggerized by Lasantha - Premium Blogger Themes | Hot Sonakshi Sinha, Car Price in India