
Laiti jicho lingekuwa risasi,basi hapa Ferguson angekuwa majeruhi,au zaidi...

Hii inajieleza yenyewe.Kama Ferdinand hatukani kimoyomoyo basi anajikaza kumtoa mtu ngeu.Ni siku Man United waliofungwa na Barca kwenye fainali ya Champions League.

Japo Rooney anafarijiana na Tevez,anaonekana mawazo yake yako zaidi kwa mshambuliaji mwenzie Ronaldo.Wachambuzi wa soka la Uingereza wanadai kwamba mara nyingi Rooney alijitoa mhanga kubadili nafasi uwanjani ili kum-accommodate Ronaldo,ambaye anatuhumiwa kuwa m-binafsi uwanjani.

Ni kama Ronaldo anaona kinachofuata-kupewa medali za ushindi wa pili-ni kuzinguana tu.

Pamoja na umahiri katika kusaka magoli,Barbatov anasifika kwa fegi.Ni mvutaji sigara sugu.Na hapa hilo jicho analompa Ronaldo ni kama la mtu aliyelowesha sigara ya mwisho kwenye pakti katikati ya mbuga ya Mikumi.

Jicho la "baba anayeelekea ukingoni kumrekebisha mwanae".
Posted in: CHRISTIANO RONALDO,MANCHESTER UNITED
Email This
BlogThis!
Share to Facebook
No comments :
Post a Comment