AHMADINEJAD AMEKUWA AKISHUTUMIWA KWAMBA AMESHINDWA KUBORESHA UCHUMI WA IRAN Kwa mujibu wa televisheni ya taifa ya Iran,Rais Mahmoud Ahmadinejad amefanikiwa kutetea nafasi yake kwenye uchaguzi mkuu uliofanyika nchini humo wiki hii.Kwa mujibu wa taarifa hizo,Ahmadinejad amepata asilimia 67 ya kura huku mgombea wa mwenye mrengo wa mageuzi,Waziri Mkuu wa zamani Mir Hossein Mousavi,akiambulia asilimia 30.
SURA YA MAGEUZI.UKURASA WA MOUSSAVI KWENYE FACEBOOK.Hata hivyo,kuna taarifa kwamba Mousavi nae anadai ameshinda uchaguzi huo.Wagombea wengine ni pamoja na mwanazuoni mwanamageuzi Mehdi Karroubi (picha inayofuata chini) na kamanda mhafidhina wa Revolutionary Guard Mohsein Rezaei (picha ya mwisho chini).

VYANZO: Kurasa mbalimbali mtandaoni
Posted in: AHMADINEJAD,IRANIAN ELECTION 2009,MOUSAVI
Email This
BlogThis!
Share to Facebook
No comments :
Post a Comment