Featured Posts

Friday, April 22, 2011

Ijumaa Kuu Njema.Tukumbuke Kwanini Yesu Aliteswa na Kufa Msalabani


Nina miaka kadhaa sijawahi kwenda kanisani.Sijisifu wala kujisikia vizuri.Kila mara ninapoongea na Baba huwa nalazimika kumdanganya kuwa siku hizi nakwenda kanisani.Ninatoka familia ya kidini hasa,na huenda leo hii ningekuwa padre kama nisingeamini kuwa sina wito.Hata hivyo,familia yetu imemtoa mmoja wetu kwa Bwana,na sasa yeye ni sista.
Mdogo wangu mpendwa,Sista Maria-Solana Chahali

Leo ni Ijumaa Kuu,siku ambayo Bwana wetu Yesu Kristo alikufa msalabani kwa ajili yetu.Nimesema sijatia mguu kanisani kwa miaka kdhaa lakini najitahidi kadri ninavyoweza kuishi kulingana na matakwa ya Bwana.Sio kwenda kanisani au kuimba mapambio kutakompatia mwanadamu uzima wa milele bali matendo.Japo ni muhimu kujumuika na waumimni wenzetu makanisani,la muhimu zaidi ni kuishi kwa mfano wa Bwana Yesu ambaye licha ya upendo wake usiomithilika alikuwa tayari kufa msalabani kwa dhambi zetu ili atuletee ukombozi.

Wakati tovuti hii inakutakia wewe msomaji mpenda Ijumaa Kuu njema,siku hii inaweza kuadhimishwa ipasavyo kwa kutafakari kuhusu upendo wa Bwana,kujitoa kwake kwa jili yetu na upeno kwa ujumla.Kama humpendi jirani yako unayemwona kila siku utakuwa mnafiki kudai unampenda Bwana mbaye hujawahi kumwona.Yesu ni upendo na amani.

4 comments:

Malkiory Matiya said...

Na kwako pia.

Yasinta Ngonyani said...

Nawe pia na msalimia Sista Maria-Solana.

EVARIST said...

Asante mdau Malkiory na asante dada Yasinta (nitawasilisha salamu kwa sista).

Masangu Matondo Nzuzullima (MMN) said...

Huu ni wakati wa kutafakari kusudi hasa la maisha yetu hapa duniani. Maisha yetu yana thamani na lengo muhimu ndiyo maana Yesu Akaja kutufia. Ni wajibu wetu basi kuwasaidia ndugu zetu wanaoteseka na kuwa kiini cha faraja na farijiko kwa wengine hapa duniani.

Ingependeza kama nini kuona kuwa mafisadi wote wanatoa zaidi ya nusu ya utajiri wao kusaidia masikini katika kipindi hiki tunapokumbuka mateso ya Mkombozi wetu. Ati hayo mabilioni yote yatawasaidia nini siku watakapokuwa kimya katika majeneza yao ya thamani?

Nakutakia Pasaka Njema kwako wewe pamoja familia yako!!!

Post a Comment

 
Design by Free WordPress Themes | Bloggerized by Lasantha - Premium Blogger Themes | Hot Sonakshi Sinha, Car Price in India